Skip to main content

JINSI YA KUGUNDUA NA KUTHIBITI VIDONDA VYA TUMBO( PEPTIC ULCER)

MAELEZO YA UTANGULIZI KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO

Tunashukuru kwa kuendelea kufatilia makala zetu, kwa maoni na ushauri ama uhitaji wa kufika ofisini basi endelea kutuandikia kwa namba 

0714206306


Kupata ufahamu mpana juu ya vidonda vya tumbo ni vema kuelewa kwanza mfumo unaohusika na tumbo ambao ni umen'genyaji wa chakula. Sehemu kuu zinazohusika katika umen'genyaji huo ni kinywa,umio ambayo ni misuli wenye urefu wa sentimeta 23 ambao huunganisha koromeo na tumbo'esophagus',mfuko wa nyongo na sehemu ya mwanzo ya utumbo mdogo'duodenum',utumbo mdogo,kongosho,utumbo mpana na sehemu ya mwishoni ya utumbo'rectum'. Mfumo wa mmen'genyo wa chakula hasa kuta za umio,tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na tindikali inayotumika kumen'genya chakula inaposhambulia kuta hizo, hii ndiyo vidonda vya tumbo'Peptic Ulcers',vidonda vya mfumo wa umen'genyaji chakula vikiwa kwenye tumbo ni 'Gastric Ulcer'vikiwa katikati ya sehemu ya mwanzo ya utumbo mdogo ni 'Duodenal Ulcer' na vikiwa katika koromeo tunaita 'Esophageal Ulcer'.

NINI HUSABABISHA VIDONDA VYA TUMBO:

 Kisababishi kikuu ni bacteria aina H.Pylori Helicobacter Pylori ambaye hupatikiana kupitia vyakula na maji,pia hupatikana kwenye mate ya binadamu hivyo inaweza kusambazwa mdomo kwa mdomo haswa kwa wenza wanaonyonyana ndimi. Bacteria hawa huishi kwenye kuta za utumbo na hutengeneza vimen'genya viitwayo. Urease inayopunguza athari za asidi kwenye utumbo,utumbo hutaka kufidia kiasi cha asidi kinachopotea kwa kutengeneza zaidi na husababisha kukwangua kuta za utumbo, idadi kubwa ya watu wenye vidonda pia wana ndugu wenye vidonda vya tumbo,uvutaji sigara na tumbaku pamoja na unywaji pombe pia husababisha vidonda na msongo wa mawazo pia.

 DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO

Ni nadra sana kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo kutoonyesha dalili kama maumivu makali ya tumbo aidha usiku.ukiwa na mawazo,ukiwa na njaa au ukishiba sana(maumivu haya huanzia kwenye kitovu na kupanda juu hadi katikati ya kifua),kushindwa kumeza chakula au kukwama kama kinataka kurudi,kujisikia vibaya baada ya kula,kupungua uzito,kukosa hamu ya kula,kutapika damu,kupata choo cheusi chenye damu,kuhisi kutapika.

JINSI YA KUGUNDUA NA KUDHIBITI VIDONDA VYA TUMBO

Maelezo ya mgonjwa kuhusu dalili humwezesha daktari kuhisi kinachomsumbua mgonjwa kuwa ni aina gani ya vidonda vya tumbo aidha peptic ulcers,gastric ulcer,duodenal ulcer au esophageal ulcer. Ili kuthibitisha aina ya vidonda vipimo vifuatavyo hufanyika
·        kupima damu kuangalia bacteria aina ya h.pylori na kama mgonjwa amekuwa akitumia antibiotic au dawa za vidonda'proton pump inhibitors-PPIs mfano. Omeprazole'vipimo vyake vya damu vitaonyesha majibu hasi.
·        kupima pumzi:mgonjwa hupewa anywe maji yenye atomi za kaboni zinazoweza kuvunjia,hii hufanya bacteria ya H.pylori kuvunjika na baada ya saa moja mgonjwa hutoa pumzi kwenye chombo kilichofunikwa na endapo mgonjwa ameambukizwa sampuli ya pumzi itaonyesha vipande vya kaboni kwenye kabonidioksaidi.
·        kupima antigeni kwenye kinyesi,kuangalia kama kuna bacteria h.pylori kwenye kinyesi
·        kufanya x-ray ya sehemu ya juu ya tumbo'upper gastrointestinal x-ray'picha huonyesha esophagus,mfuko wa tumbo'stomach'na duodenum


JINSI YA KUISHI NA VIDONDA VYA TUMBO
 Baada ya kufahamu kwa kina vyanzo vya vidonda vya tumbo,aina ya vidonda vya tumbo,dalili ya vidonda vya tumbo,uchunguzi/vipimo ni vyema tufahamu mambo yatakayotusaidia kuishi vizuri tukiwa na vidonda vya tumbo.
·        Awali ni vyema mhanga aache kabisa kutumia kahawa na chai kwani huongeza kiwango cha asidi kinachotenezwa na tumbo lako(unaweza kutumia mchaichai kama mbadala).
·   
·        Jitahidi kupunguza uzito hasa ikiwa uzito umezidi na hauendani na kimo chako.
·        Kula angalau kidogo mara kwa mara,hii itasaidia kupunguza athari za asidi inayotengenezwa na tumbo.
·        Epuka kunywa pombe na vileo kwani hutonesha kwenye vidonda vinavyotaka kupona.
·        Epuka matumizi ya viungo vya vyakula kwani yana gesi/asidi nyingi,Acha kabisa kuvuta sigara kwani hukuweka kwenye hatari zaidi ya vidonda kuanza upya au kuzuia vidonda.
Mpenzi msomaji wa makala hii yawezekana wewe ama ndugu ama rafiki yako ni mgonjwa na anasumbuliwa na tatizo hili, na ametumia madawa mengi bila kupona. Basi napenda kukupa habari njema kuwa tumefanikiwa kutengeneza vidonge kwa kutumia mimea ambayo inatibu na kuondoa tatizo hili.
dawa zetu za mimea zinatumika kwa week 4 .

Dawa ni Tsh 150,000/=


kama upo mkoani basi usihofu maana utatumiwa dawa baada ya kufanya malipo.


Usiache kufatilia makala inayofuata: Fahamu jinsi bacteria wa H.pylori wanavosababisha vidonda vya tumbo.

Comments

Popular posts from this blog

KUTOKWA NA UCHAFU UKENI, CHANZO NA TIBA YAKE

Uke wa mwanamke hufanya kazi ya kutoa njia kati ya sehemu ya nje ya mwili na viungo vya uzazi vya ndani vya mwanamke. Hali ya kawaida ya majimaji yaliyomo katika uke wa mwanamke huwa ni ya tindikali ili kuzuia maambukizi ya vijidudu wa kuleta maradhi. Hali hii ya utindikali huletwa na bacteria waishio katika uke wa mwanamke. Bacteria hawa ni wa kawaida na hawana madhara kwa mwili. Uke ulio katika hali nzuri hutoa majimaji haya ili kujisafisha. Majimaji haya yanayotengenezwa katika uke na kwenye eno la cervix hufanya kazi ya kuondoa seli zilizokufa na bacteria waharibifu nje ya mwili na huu ndio uchafu wa kawaida ambao mwanamke hutoa ukeni. Kutoa uchafu huu sehemu za siri ni njia ya kuusafisha uke na kuzuia maambukizi ya magonjwa. Kitu cho chote ambacho kitaharibu uwiano wa utengeneaji wa majimaji haya ndani ya uke kinaweza kujenga mazingira ya maambukizi katika uke. Uchafu Wa Sehemu Za Siri  Wa Kawaida Wanawake wote hutoa uchafu sehemu za siri. Kiwango cha uchafu unaotoka, ra

JINSI YA KUONGEZA UFANISI WA VICHOCHEO VYA KIUME (TESTOSTERONE) NA KUKINGA DHIDI YA MATATIZO YATOKANAYO NA KUKUA KWA TEZI DUME KWA KUTUMIA VYAKULA HIVI VI 5

Maelezo ya utangulizi. Kichocheo cha testosterone, japo huusishwa zaidi na upande wa mwananume ni muhimu kwa afya ya pande zote mbili yaani mwanamke na mwanamme pia.kadiri umri unavoenda mbele basi kiwango cha uzalishaji wa kichocheo cha testerone kupungua, kupungua kwa kichocheo hiki kunaambatana na ukuaji wa tezi dume (prostate gland),kupotea kwa nywele na pia saratani mfano saratani ya tezi dume. .KAZI KUBWA YA KICHOCHEO HIKI NI KUONGEZA MSUKUMO NA HAMU YA TENDO LA NDOA , KUIMARISHA MISULI NA MIFUPA MWILINI. NINI KINAHITAJIKA ILI KUZALISHA KICHOCHEO CHA TESTOSTERONE? Ili kuhakikisha uzalishaji wa kichocheo cha kiume unafanyika, mwili unahitaji virutubisho au viini lishe mbalimbali, baadhi ya viini lishe hivyo ni madini ya ZINC na vitamin D3,  vitamini D inaweza kuzalishwa na mwili pale ngozi yako inapokutana na mwanga wa jua, hapa nazungumzia mwanga wa asubuhi wakati jua ndo linachomoza na pia lile jua la jion karibia na kuzama, hivyo utakubaliana na mimi kuwa wengi wet

MADHARA YA PUNYETO NA TIBA YAKE

MAELEZO  YA AWALI KUHUSU TATIZO LA UPIGAJI PUNYETO Watu wengi sana wanataka kufahamu jinsi gani wafanye ili kuachana na kitendo cha upigaji punyeto. Punyeto ni tendo la mtu la kuamsha hisia za mapenzi au msisimko ambao unampelekea mtu huyu kufikia kilele cha kujimalizia tamaa zake! Bila kufanya tendo halisi, hutumia fikra zake katika picha za zinazoitwa za ngono au picha zozote zinazoweza kulifanikisha tendo hilo, movie n.k. Kilele cha yote anafikia mahali anajimalzia tamaa zake mwenyewe!. Nimekuwa nikiona baadhi ya watu wanaosema wameelimika wakipingana wao kwa wao katika suala zima la kupiga punyeto! Wako wanaotetea kutokana na elimu yao na wanasema kwa ujasiri mkubwa kwamba "kupiga punyeto ni sehemu ya maisha ya mwanadamu" Ina maana katika maisha ya mwanadamu upigaji punyeto inaelezwa ni kama tendo la lazima mpaka inafikia mahali wanasema ni sehemu ya maisha (Maisha) ya mwanadamu. Nimekuwa nikipata kesi nyingi sana juu ya madhara yatokanayo na punyeto. Aslimia 60